Ibrahim Traore: Habari potofu zinazotumiwa kumtukuza

Ibrahim Traore: Habari potofu zinazotumiwa kumtukuza



Mamia ya video zinazotolewa na AI zikimuonesha kiongozi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traoré, kama shujaa wa Afrika nzima, nyingi zikiwa na taarifa za uongo, zimekuwa zikijaa kwenye mitandao ya kijamii kote Afrika na Kusini mwa Jangwa la Sahara tangu mwishoni mwa Aprili.

Je zimekuwa na ukweli kwa kiasi gani?

@sammyawami anaelezea

#bbcswahili #burkinafaso #ibrahimtraore

Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili

20 thoughts on “Ibrahim Traore: Habari potofu zinazotumiwa kumtukuza

  1. Hakuna habari ya BBC itaandika fahari ya Africa.
    Zaidi wataandika Africa yenye njaa ,wataandika wamesaidia ila misaada ya magharibi inachekesha sana. Wakimbizi nk. Hawawezi kamwe kueleza mafaniko. Habari zote za BBC kwa sasa siziamini kabisa. Mpaka nipate kwa chombo huru cha eneo husika.

  2. Nyie BBC nimeanza kuwachukia kumbe Traore aliongea kweli kuwa hivi ni vyombo vya Habari vya hovyo na wapotoshaji wakubwa kwa Africa!sasa nimeamini kuwa Mwamba yupo sawa kabisa kwa aliyo yasema ni ya kweli na yamewaumiza sasa kwa kuwa mmeambiwa ukweli na nyie mmeamua kutoa hadharani chuki zenu kwake!!Africa sasa tunajua ukweli hamuwezi kutudanganya tena nyie wapuuzi!!

  3. Nimepata hadi hasira, yaani na ww kumbe nilivyokuwa nakutizama kumbe ni walewale kasoro mkia, kaa kimya acha kutupotosha watu, acha kutupotoshea baadhi ya waAfrica wasioelewa nn mnakiandaa, mnatengeneza propaganda zenu za kijinga mkidhani tutaingia kingi, haya hao mabwana zako walifanya nini hapo buk'faso!? Zaidi ya kujinufaisha wao? Wajinga kama nyinyi nikiwaona mnakata roho kisa kiu ya maji nakumalizia na gundi

  4. Una sauti nzuri sana lakini amna mtu asiyejua kuwa mnatumika watu weusi mnatumika vibaya na vyombo vya habari vya magharibi kudanganya waafrica na ulimwengu kiujumla tafuta kazi nyingine kama salimu kikeke bro acha kutumika kipumbavu na watu wa magharibi

  5. You're nothing to say that
    Sijui wanakulipa shilling ngapi
    Mbona black hampendi maendeleo ya black wenzenu mnatumiwa kujichafua wenyewe Kwa wenyewe,
    ACHA KUPOTOSHA WATU WA AFRICA
    KWA UAFRICA WAKO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *