Ibrahim Traoré ‘Shujaa wa Burkina Faso’

Ibrahim Traoré ‘Shujaa wa Burkina Faso’



Inasemekana alikuwa mnyenyekevu lakini mwerevu shuleni, Kapteni Ibrahim Traoré wa Burkina Faso ni afisa wa jeshi ambaye alichukua madaraka kwa mapinduzi katika moja ya makoloni ya zamani ya Ufaransa huko Afrika Magharibi mwaka 2022.

Alimpindua aliyekuwa mshirika wake, Luteni Kanali Paul-Henri Damiba, baada ya kumtuhumu kwa kushindwa kutimiza ahadi yake ya kukomesha uasi wa Waislamu ambao umekikumba Burkina Faso tangu 2015.

Amekuwa akifanya mabadiliko nchini humo na wananchi wakionesha kumkubali. Je ni mabadiliko gani?

Lizy Masinga anaelezea



#bbcswahili #burkinafaso #IbrahimTraore #mapinduzi #uongozi #Damiba
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili

39 thoughts on “Ibrahim Traoré ‘Shujaa wa Burkina Faso’

  1. Huyu ni mwamba magufuli wa 2 tunamuombea mungu asimame na aongezewe miaka 30 yakuongoza mana alitangaza wanachuo kulipwa wafungwa kupunguziwa kifungo kwa kufanya kazi yakulima je mnaona huyu ana utani ? Amepewa mwaliko na marekan akakataa wakat wa uhapisho wa tramp mana anajua madhara yakwenda uko ataenda kupandishwa lory na pamoja mana Africa hatudhaminiwi ata tone huyu ni mwamba aaaaaa

  2. Traole ni mzalendo na nchi yake anaipigania sana ili wajikomboe na kua tegemezi tunaweza mfananisha na Hayati muamar Gadaffi na magufuli yaani wanatumia rasilimali za nchi kwa ajili ya wananchi hongera sana shujaa wetu.

  3. Wajifunze na nchi zingine za Africa,,kwani hakuna maoni ya waafrica wote tupige kura kumpigia kura Rais anaefanya vizuri na kukubaliwa zaidi hata nje ya mipaka yake ,Basi baada ya kura hizo akionekana wengi wanamkubali basi iwekwe SHERIA ,WOTE BARANI AFRICA TUNAFUATA NYAYO ZAKE,,kwasababu ukisema kila mmoja ajiendee vile nikiongozi kwa nchi yake ,HAWABADILIKI,maana hata Waafrica Wengine WANAMPINGA HUYU MWAMBA.

  4. Isingekuwa rahic kumponda kwa sasa ikiwa Africa nzima inampenda ila tunajua Baadae mtatuletea na habari za kumchafua pia. DON'T TRUST BBC ANYMORE

Leave a Reply to @faidaimmaculee28 Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *